Biashara ya Kitanzania
Zaidi ya Duka la Vifaa — Sisi ni Sehemu ya Familia Yako.
Kwa muongo mmoja, tumekuwa chaguo la kwanza la Watanzania kwa kusambaza vifaa halisi vya kielektroniki kutoka kwenye brand kubwa duniani. Hatuuzi tu bidhaa; tunarahisisha maisha yako.
Historia Yetu
Tumejengwa Kukuhudumia Vizuri Zaidi
Kila biashara imara ina asili inayotoka moyoni. Jina 'Jaden' lilibeba maana mpya kabisa kwenye maisha yetu baada ya kubarikiwa kupata mtoto wa kiume. Ujio wake ulitupa msukumo mkubwa wa kujenga kitu chenye thamani, kinachodumu, na kinachotunza familia. Tukiongozwa na msukumo huo, Jaden Home Store ilizaliwa. Kile kilichoanza kama ndoto ya kifamilia, leo hii kimekuwa kitovu cha usambazaji wa vifaa vya kielektroniki vinavyoaminika Tanzania nzima. Kwa miaka 10 ya uzoefu, tunajivunia kuwa daraja linalokuunganisha wewe na ubora usio na mashaka wa Hisense, Samsung, LG, TCL, na JBL. Nyumba yako ndio msingi wako — na sisi tuko hapa kuhakikisha inapata kilicho bora pekee.
Mtandao Wetu
Matawi Yetu
Tunakufikia popote ulipo
Makao Makuu
Sinza
Tawi
Kariakoo
Tawi
Mwanza
Tawi
Dodoma
Makao Makuu: Sinza Africa Sana, Dar es Salaam — 0655 285 158 Kariakoo, Dar es Salaam — 0672 809 928 Mwanza — 0657 972 572 Dodoma — 0713 901 212
Kwa wanaonunua mtandaoni, mzigo wako unakufikia salama mpaka mlangoni.
Tunu Zetu
Misingi Inayotuongoza
Big Brands, Best Distributor
Tunafanya kazi moja kwa moja na watengenezaji. Unaponunua kwetu, unanunua uhakika, uimara, na amani ya moyo kwa bidhaa zenye warranty kamili.
Uzoefu Unaolipa
Hatukuanza jana. Miaka kumi kwenye soko ina maana tunaelewa haswa kile ambacho Mtanzania anakitafuta: ubora wa kiwango cha juu unaoendana na thamani halisi ya pesa yako.
Mtandao Mpana Nchini
Iwe uko Dar es Salaam, Mwanza, au Dodoma, Jaden Home Store iko karibu nawe. Na kwa wanaonunua mtandaoni, mzigo wako unakufikia salama mpaka mlangoni.
Tembelea Duka Letu Leo
Gundua kwanini wateja wanachagua Jaden Home Store kama sehemu yao ya kuaminika ya ununuzi.